Habari za michezo

‘KIPENSI’ CHA RONALDO CHAZUA GUMZO MTANDAONI…KOCHA MAN UTD AMKAZIA KUSEPA ‘OT’…CHELSEA WAMKATAA…

admin July 16, 2022 10:11 am


Cristiano Ronaldo amevunja ukimya baada ya kutuma picha kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa amevalia jezi ya kaptula ya Manchester United huku akifanya mazoezi.

Picha hiyo imemuonyesha Ronaldo akiwa bize na matizi ‘Gym’ licha ya kukosa ziara ya Man United, ya kujiandaa na msimu mpya kutokana na matatizo ya kifamilia.

Aidha mashabiki wametabiri huenda Ronaldo akabaki, baada ya kuvaa kaptula ya Man United,  iliyoashiria mambo mengi kuhuhu hatima yake.

Licha ya Ronaldo kuweka wazi hana mpango kukipiga Old Tafford kocha wa Ma United, Erik ten Hag amesisitiza staa huyo hauzwi na ataendelea kuwepo kwaajili ya msimu huu unaokuja.

Wakati huo huo Thomas Tuchel amesema Chelsea haina mpango wa kumsajili Ronaldo, baada ya kuhusishwa na nyota huyo wa Kimataifa wa Ureno.

AUSSEMS AZIVURUGA KLABU ZA KENYA NA RWANDA….ADAIWA KUSAINI MKATABA BILA KUAGA… JAMBO LA SIMBA LATIKI MISRI…’MAVITUZ’ YA KOCHA MPYA SIO POA…MASTAA WANYOOSHWAAA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply