Habari za michezo
USAJILI SIMBA WAMSONONESHA TUNDA MAN….ADAI YUKO TAYARI KUTEMBEZA BAKULI LA KUPATA PESA ZA USAJILI…
Msanii na shabiki wa Klabu ya Simba Tundaman amesema yupo tayari kupitisha bakuli la kuchangia timu yake kufanya usajili mkubwa kama walivyozoea.
“Katika asilimia 100 Simba wamenifurahisha kidogo tu kama asilimia 4, viongozi wangu nina wito hapa kama wamefeli vibunda hawana weseme Tundaman kuna jukwaa Mwanza nafanya show hata za bukubuku kuchangia mchezaji fulani”.
“Nipo radhi kupitisha bakuli Simba sisi ndio wenye timu” ameongeza Tundaman
Mpaka leo , Simba imetambulisha wachezaji wawili tu wa Kimataifa akiwemo Straika Moses Phiri na Kiungo mshambuliaji Augustine Okrah

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.