Habari za michezo

KUELEKEA FAINAL ZA CHAN…TAIFA STARS WAANZA ‘MBILINGE MBILINGE’ ZA MAANDALIZI…..’SOPU’ KAMA KAWAIDA NDANI YA NYUMBA..

admin July 17, 2022 7:16 am


WACHEZAJI  wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameanza maandalizi kwa ajili ya michezo ya kufuzu CHAN 2023.

Stars inayonolewa na Kocha Mkuu,Kim Poulsen inatarajiwa kucheza mechi mbili ndani ya mwezi huu wa Julai kuwania kufuzu CHAN.

Itakuwa mchezo dhidi ya Somalia ambapo ule wa awali unatarajiwa kuchezwa Julai 23 na ule wa pili unatarajiwa kuchezwa Julai 30,2022 katika Uwanja wa Mkapa.

Jana Julai 16,2022 Taifa Stars imeanza mazoezi kwenye uwanja wa Uhuru kujiandaa na michezo hiyo muhimu.

Miongoni mwa mastaa ambao walikuwa kwenye kikosi ni pamoja na Aishi Manula,Metacha Mnata,Kennedy Juma,Relliats Lusajo,Abdul Suleiman,’Sopu’.

BAADA YA KASEKE, BALAMA NA YAASSIN KUPIGWA CHINI YANGA….MASTAA WENGINE WALIOKALIA KUTI KAVU HAWA HAPA…. KUELEKEA MSIMU UJAO… SIMBA KUJIPIMA NGUVU NA TIMU YA TAIFA YA MISRI…MCHONGO MZIMA UKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply