Uongozi wa klabu ya Yanga, umeahidi kutorudia makosa katika michuano ya kimataifa kwa kujipanga vyema na kuhakikisha wachezaji wapya wanapata vibali mapema vitakavyowaruhusu kucheza michuano ya Klabu bingwani barano Afrika.
Yanga tayari imejihakikishia kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Msimu uliopita, Yanga iliwakosa baadhi ya wachezaji wa kimataifa kutokana na kuchelewa kupata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) akiwemo Khalid Aucho.
Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Yanga Haji Manara, amesema msimu uliopita timu yao ilishindwa kufanya vizuri baada ya wachezaji wao tegemeo kuchelewa kupata ITC.
”Tayari wamejifunza katika hilo, hiyo ndio sababu ya kukamilisha usajili wao wa wachezaji wapya mapema ili kuhakikisha wote wanakuwepo katika kikosi chao” amesema Haji Manara.