Habari za michezo

RASMI….MATAJIRI WAPYA LIGI KUU WAMALIZANA NA DEUS KASEKE JUMLA JUMLA…

admin July 23, 2022 10:16 am


KLABU ya Singida Big Stars imetangaza rasmi kunasa saini ya aliyekuwa kiungo wa Yanga, Deus Kaseke kwa mkataba wa miaka miwili.

Kaseke aliachana na Yanga Julai 14 mwaka huu baada ya mkataba wake na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara Yanga kufikia ukomo.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2015 alishindwa kuongezewa mkataba mpya kutokana na kushindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara chini ya Kocha mkuu Nasreddine Nabi huku akicheza zaidi akitokea benchi.

Kaseke ambaye ameitumikia Mbeya City na Singida United anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Yanga kujiunga na timu hiyo baada ya awali kutangazwa mabeki, Paul Godfrey ‘Boxer’ na Yassin Mustapha ambao nao walitemwa.

Mbali na mastaa hao ila Kaseke anaungana na Kelvin Sabato aliyetoka Mtibwa Sugar, Metacha Mnata (Polisi Tanzania), Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Said Ndemla (Mtibwa Sugar) na Benedict Haule wa (Azam FC).

WAKATI YANGA WAKIJICHIMBIA KIGAMBONI….GEITA GOLD WAIIZIDI MAARIFA….WAENDA NNJE YA NCHI KUWEKA KAMBI…. AKPAN AKABIDHIWA ‘VIRAGO’ VYA PASCAL WAWA SIMBA….TIKITAKA ZA USAJILI ZAMTOA MWENDA KWA MKOPO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply