Habari za michezo

SALEH JEMBE AKAZIA HUKUMU YA TFF KWA MANARA…ADAI MARAFIKI WANAFKI WANAMJAZA UPEPO KUWA HANA MAKOSA…

admin July 23, 2022 4:00 pm


Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Saleh Ally ‘Jembe’ amesema Haji Manara anapaswa kujiweka mbali na marafiki wanafiki ambao wanamjaza upepo (Kumdanganya) kwamba hana makosa kutokana na hukumu aliyoipata ya kufungiwa miaka miwili kutojihusisha na soka pamoja na faini ya shilingi milioni 20.

Akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa habari wa Global TV, Jembe amenukuliwa akisema:

“Mimi natakuwa tofauti na rafiki zake wengine wote, natakakuwa tofauti na rafiki zake especially rafiki zake wanafiki rafiki ambao badala ya kumuambia kitu sahihi cha kufanya wanazidi kumpoteza zaidi kwa kufuata masuala ya kishabiki.

“Tunaona kweli Haji amekosea na kama amekosea imefikia hatua Haji amehukumiwa hatuwezi kuwa watu wazuri kama tutakuwa tunafurahia kuhukimiwa kwa Haji badala yake tunatakiwa kuwa watu ambao tunatakiwa kumueleza ukweli.”

Aidha, Jembe amemtahadharisha Manara kuhusu kutaka kushindana Mamlaka ya soka nchini kwani kwa kufanya hivyo hawezoi kufanikiwa kwa lolote na hakutakuwa na manufaa au afya kwa maendeleo ya soka nchini.

Jembe amemshauri Manara kujitathmini na kuzingatia maelekezo ya Mamlaka ya soka kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kutengeneza mazingira ya yeye kuja kusamehewa baadaye.

Amesema tayari kuna ushahidi wa watu wengi ambao walishawahi kufungiwa na baada ya kuonesha mwenendo mzuri wakafunguliwa vifungo vyao na mmoja wapo ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela.

BOSI AZAM FC AFUNGUKA WALIVYOHANGAISHWA KUPATA SAINI YA SOPU…AFUNGUKA A-Z SIMBA NA YANGA ZILIVYOSUMBUA… WAARABU WAIPA SIMBA KIFAA…NI MBADALA WA SAKHO…MASTAA WAMSUBIRISHA NABI YANGA…KAMBOLE APEWA JEZI NGUMU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply