Habari za michezo

WAKATI WENZAO WAKIWA KWENYE TIZI KALI…UONGOZI YANGA WAFUNGUKA A-Z WALIPO BANGALA NA MORRISON..

admin July 27, 2022 2:23 am


Uongozi wa Yanga umethibitisha kuchelewa kujiunga kwa mastaa wao wawili, Bernard Morrison na Yanick Bangala kutokana na sababu mbalimbali.

Yanga tayari wameanza mazoezi ya kujiweka fiti kujiandaa na msimu mpya wa ligi sambamba na mashindano ya kimataifa wakiiwakilisha nchi Klabu bingwa.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema wachezaji wote wamewasili kambini isipokuwa Bangala na Morrison ambao hadi alhamisi watakuwa wameungana na wenzao kwenye mazoezi.

“Mastaa hao taarifa za kuchelewa kwao zinafahamika lakini wote watawasili kesho na alhamisi wataanza mazoezi pamoja na wenzao ili kujiweka witi kuelekea msimu mpya,” alisema na kuongeza;

“Ni wachezaji watano ambao walichelewa kujiunga na kambi ambao ni Khalid Aucho ambaye jana kaanza mazoezi, Fiston Mayele na Shaban Djuma ambao wataanza mazoezi leo baada ya kuwasili jana.”

LIVE KUTOKA AVIC…MAMBO KAMA MBELE..NABI ATAMBA YANGA INA WATU…ZORAN ADAI SIMBA INAANZA UPYAAA… SAKATA LA KUFUNGIWA NA TFF….MANARA AFUNGUKA MAPYA…ADAI HATAKI HURUMA YA MTU…YUPO TAYARI KUFUNGWA MIAKA 10…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply