Home Habari za michezo BAADA YA KIMYA KIREFU….HATIMAYE JINA LA NCHIMBI KUTAJWA TENA LIGI KUU AKIWA...

BAADA YA KIMYA KIREFU….HATIMAYE JINA LA NCHIMBI KUTAJWA TENA LIGI KUU AKIWA NA TIMU HII MPYA…

 


Winga wa zamani wa Yanga na Geita Gold, Ditram Nchimbi anatajwa kujiunga na Tanzania Prisons iliyonusurika kushuka daraja ili kuongeza nguvu kikosini.

Prisons ilibaki Ligi Kuu kufuatia ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Play Off, ambapo Ijumaa ya wiki hii itakuwa kambini kujiandaa rasmi na msimu ujao.

Hata hivyo timu hiyo ya jijini Mbeya ipo kwenye mawindo ya kusaka nyota nane wapya ikiwa ni makipa wawili, Straikia, beki wa kati na winga mmoja akiwa na jukumu la kutengeneza krosi za mabao.

Chanzo cha ndani ya klabu hiyo, kimedokeza kuwa nyota huyo aliyewahi kuzitumikia timu kadhaa ikiwamo Mwadui, Polisi Tanzania, Yanga na Geita Gold huenda akamalizana nao muda wowote.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO Vs NAMUNGO YA MGUNDA....'NONDO' KALI ZA SIMBA HIZI HAPA...