Home Habari za michezo BAADA YA KUUPATA URAIS YANGA….INJINIA HERSI KUANZA KAZI RASMI LEO…KAMBI YA MAREKANI...

BAADA YA KUUPATA URAIS YANGA….INJINIA HERSI KUANZA KAZI RASMI LEO…KAMBI YA MAREKANI YATUPWA…SAFARI NI KARATUUU…


KIKAO cha kwanza cha Yanga chini ya rais mpya mhandisi, Hersi  Said kinatarajia kufanyika leo, kati za ajenda zilizotajwa zitapewa nafasi ya kujadili ni klabu hiyo itaweka kambi wapi, kujiandaa na msimu ujao (2022/23).

Awali Yanga ilitarajia kuweka kambini nchini Marekani, ambapo taarifa  zinasema kocha Nasreddine Nabi hajakubaliana na hilo, akitaka itafutwe sehemu ya karibu ili kupata muda mwingi wa kuiandaa timu.

Umetajwa mkoa wa Karatu ambao ndio pendekezo la Nabi, pia nchi ya Uturuki wanayotaka viongozi, hivyo katika kikao hicho kinaweza kuamua ni wapi Yanga itaweka kambi kwa ajiri ya msimu ujao.

“Msimu ulioisha kocha Nabi hakupendezewa kuweka kambi nje ambako hakupata muda mwingi wa kukiandaa kikosi na akiangalia muda mchache aliyonao kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Ligi Kuu ijayo anaona kwenda Marekani watapoteza muda mwingi,” alisema mmoja wa kiongozi wa timu hiyo.”

Aliongeza “Ombi la Nabi kutokwenda Marekani limekubarika, ila la kwenda Karatu ndilo linajadiliwa.”

Tangu Hersi achaguliwe kuwa Rais wa Yanga hicho kitakuwa kikao chake cha kwanza, kitakachotoa picha nzima ya nini ataanza nacho baada ya kuingia madarakani.

Yanga ilifanya uchaguzi Julai 9 uliyomsimika Hersi madarakani na aliyekuwa mwenyekiti dokta Mshindo Msolla kuachia ngazi.

SOMA NA HII  KIMENUKA CHAMAZI.... KISA KUMTUSI MENEJA.... AZAM FC KUWAFUKUZA AGGREY MORRIS, 'SURE BOY'..