Home Habari za michezo KIUNGO YANGA ALAMBA SHAVU TIMU YA LIGI KUU UGIRIKI…..AOMBEWA DUA ASIPATE MAJERAHA…

KIUNGO YANGA ALAMBA SHAVU TIMU YA LIGI KUU UGIRIKI…..AOMBEWA DUA ASIPATE MAJERAHA…


Kiungo fundi wa mpira wa timu ya wanawake ya Yanga Princess, Fatuma Ibrahim ‘Fetty Didier’ amelamba shavu baada ya kusajiliwa na klabu ya soka ya Neesatromitou iliyopo Ugiriki kwa mkataba wa miaka miwili.

Fetty alikuwa mmoja ya nyota walioiwezesha Yanga kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), nyuma ya mabingwa Simba Queens na Fountain Gate Princess.

Kupitia ukurasa wa klabu hiyo ya Ugiriki ilimtambulisha rasmi Fetty kujiunga kuitumikia timu hiyo.

“Usajili wa kwanza kimataifa kwa msimu wa 2022-2023, Fatuma Mwisendi amekamilisha nyaraka zote na kusaini, kilichobaki ni kutangazwa rasmi,” ilisema taarifa ya klabu hiyo

“Fetty anayecheza kama kiungo mchezeshaji na mkabaji, nahodha wa Yanga Princess inayoshiriki Ligi Kuu na timu ya Taifa Tanzania karibu kwenye kundi, tunakutakia mafanikio mema bila kupata majeraha.”

Upande wa Fetty alishaaga Yanga Princess katika ukurasa wake wa Instagram akiandika: “Kwa muda wote niliowatumikia daima nimejifunza mengi.

“Mmenikomaza kwa hali zote nilizokutana nazo na tulifurahi pamoja na kuhuzunika pamoja. Daima mtabaki kuwa sehemu ya familia yangu.”

Yanga Princess inakuwa ni mara ya pili kutoa mchezaji kwenda nje ya nchi msimu huu baada ya kumuuza Aisha Masaka kwenda BK Hacken ya Sweden, japokuwa alishindwa kuitumikia kutokana na kuwa majeruhi.

Ligi Kuu ya Wanawake imeanza kuwa na msisimko wa aina yake.

SOMA NA HII  SIMBA vs USGN...HAIJAWAHI KUTOKEA..MO AONGEZA MZUKA..ZAHERA AWAPA MSALA YANGA...