Home Habari za michezo KUELEKEA SIMBA DAY….KIBADENI AIBUKA NA HILI JIPYA…ATOA KILIO CHA WACHEZAJI WAKONGWE…MGOSI AKAZIA…

KUELEKEA SIMBA DAY….KIBADENI AIBUKA NA HILI JIPYA…ATOA KILIO CHA WACHEZAJI WAKONGWE…MGOSI AKAZIA…


Tamasha la Simba Day Agosti 8, litatoa mwanga wa nini malengo ya klabu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara inayoanza Agosti , kwa mujibu wa mastaa wa zamani wa timu hiyo.

Aliyewahi kuichezea klabu hiyo na kuifundisha, Abdallah Kibadeni alisema anachotamani kukisikia siku hiyo ni kuona wachezaji watakaounda timu hiyo.

“Usajili wa msimu huu umekuwa wa siri, kuna wachezaji walitajwa kuachwa na wengine kuongezwa, uhakika zaidi wa kipi ni kipi utapatikana siku hiyo,” alisema Kibadeni na kuongeza;

“Jambo lingine mwaka huu wasiwasahau wachezaji wa zamani ambao wametoa jasho lao kuhakikisha inakuwa Simba hii ya sasa, wapewe heshima yao katika tamasha hilo, wapo wazee wengi kama kina Hassan Dalali, mimi mwenyewe angalau wakumbukwe na ikiwezekana tuwe wageni kuliko kuwaleta kutoka nje.”

Kwa upande wa nahodha wa zamani wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi aliwahamasisha mashabiki wa Simba kujitokeza wa wingi ili kuuanza msimu kwa vaibu la kutosha.

“Tamasha la msimu huu litumike kuzika maumivu ya msimu uliyoisha na kuwapa morali wachezaji ili kujua tupo pamoja nao, hatutakiwi kuanza ligi kinyonge,” alisema. Simba Day ya mwaka huu itakuwa ya 13 tangu ilipoanzishwa 2009 chini ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali.

SOMA NA HII  SAKATA LA GSM NA UDHAMINI WA LIGI KUU...SIMBA WAIBUKA NA HILI JIPYA...WANASHERIA WAFICHUA MADUDU ZAIDI..