Home Habari za michezo HIVI NDIVYO PACOME ANAVYOTUMBUA MSHAHARA WA YANGA KISHUA….

HIVI NDIVYO PACOME ANAVYOTUMBUA MSHAHARA WA YANGA KISHUA….

Habari za Yanga leo

PACOME Zouzoua ‘Zizzou’ anaupiga mwingi uwanjani akiwa na kikosi cha Yanga, akiifungia mabao manne katika Ligi Kuu Bara na matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku mashabiki wakimtambua zaidi kwa muonekano wake kichwani akiwa amepaka blichi inayomtofautisha na wenzake wa Yanga.

Sasa kama hujui ni kwamba kiungo mshambuliaji huyo kutoka Ivory Coast kila wiki jamaa anatumia zaidi ya Sh100,000 kila wiki na siri imefichuliwa na kinyozi anayemnyoa na kumpaka blichi hiyo.

Akizungumza  katika mahojiano maalumu, kinyozi huyo wa Pacome anayefahamika kwa jina la Msukuma amefichua thamani ya fedha anazotumia staa huyo wa Yanga aliyesajiliwa msimu huu kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kwa mujibu wa kinyozi huyo amesema Pacome ananyoa kila baada ya wiki moja ambapo hulazimika kutumia zaidi ya Sh100,000 za Kitanzania.

Ukipiga hesabu hiyo, Pacome ili aendelee kuonekana kama alivyo sasa, inamlazimu kwa mwezi mzima kutumia Sh400,000 na kwa hesabu za mwaka kichwa pekee yake kinamgharimu karibu Sh 4.8 Milioni pesa ambazo zinaweza kuwalipa mishahara vijana 20 wa Sh240,000 kila mmoja.

Msukuma amesema aliunganishwa na Pacome kupitia mteja wake aliyemuonyesha akaunti ya Instagram anayotumia kutuma kazi zake ndipo staa huyo akachagua staili yake.

Kinyozi amesema kuwa mwanzoni, Pacome hakuwa na mwonekano ule kwani rangi aliyokuwa nayo haikuwa na mvuto kabisa ndipo alipoamua kumbadilisha na kuwa vile alivyo sasa.

“Pacome ameonekana akivutiwa na mtindo wake, lakini ameongeza wateja zaidi kwani mastaa wana nguvu kubwa ya ushawishi kwani wanaonekana na watu wengi na kiukweli ananilipa vizuri sana.”

Nyota huyo amekuwa mmoja ya mastaa wanaotegemewa na Yanga kwa sasa kwenye michuano mbalimbali akishirikiana na wengine aliowakuta ama kusajiliwa msimu huu akiwamo Maxi Nzengeli, Yao Kouassi, Stephane Aziz KI, Diarra Djigui, Khalid Aucho na wakali wengine wazawa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA MAMELOD....KWA HILI YANGA 'MMEPUYANGA' SANA ...