Home Habari za michezo MANARA AENDELEA KUTESEKA NA ADHABU YA TFF….AIBUKA NA HOJA YA SIKU YA...

MANARA AENDELEA KUTESEKA NA ADHABU YA TFF….AIBUKA NA HOJA YA SIKU YA WANANCHI….ADAI HAMJUI YEYOTE TZ…


Siku moja mara baada ya kufungiwa na Kamati ya Madili ya TFF, Msemaji wa Yanga, Haji Marana ameibuka na ujumbe mreefu katika ukurasa wake wa Instagram akisema tatizo ni tamasha hilo.

Japo hajafunguka moja kwa moja kama anailenga kamati hiyo lakini video aliyoiweka, imeashiria tatizo lilihusiana na Siku ya Mwananchi maana video hiyo inatangaza tamasha hilo.

Huu hapa ujumbe wake aliouambatanisha chini ya video hiyo:

“Kumbe Tatizo ni hili? Uhhhh lalalaah!!! Wamebugi kwangu, Sitawaacha Wananchi,,na litakuwa Tamasha kubwa kuliko walivyodhamiria. Simjui yoyote nchi hii anaenisogelea kwa kufuatiliwa ktk Instagram ,kwa Watu wa football na Sports kwa ujumla kunizidi, nguvu hyo niliojaaliwa na Mungu,ntaitumia effectively kulipush hili Concert kuu la kisoka,, Ikiwa Parade yetu ilivunja Rekodi why tushindwe hili? Msifadhaike hata kidogo, tuombe uhai tu coz dhuluma huwa haina mwisho mwema na always haki hushinda ni suala la muda tu. Nb: Sipoi hata tone na tabu ipo pale pale, sanasana ndio itazidi, otherwise waje kuniua. Yanga Bingwa na mimi ndio Bugati Byuti Byuti”

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING: YANGA WATATURUDISHA KWENYE RELI, MASHABIKI NJOONI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here