Home Habari za michezo METACHA MNATA AZUA YA KUZUA ….POLISI TANZANIA WAIBUKA NA KUMNG’ANG’ANIA BAADA YA...

METACHA MNATA AZUA YA KUZUA ….POLISI TANZANIA WAIBUKA NA KUMNG’ANG’ANIA BAADA YA KUSAINI TIMU INGINE…


Siku chache baada ya Singida Big Stars (SBS) kumtangaza kipa Metacha Mnata kama mchezaji wao kwa ajili ya msimu wa 2022/23, Polisi Tanzania wameibuka na kuthibitisha kipa huyo ni mchezaji wao halali.

SBS imepanda daraja msimu huu na hadi sasa imesajili wachezaji sita kwa ajili ya kuongeza nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Makamu Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Robert Munis alisema Metacha ni mchezaji wao halali kwani bado ana mkataba wa mwaka mmoja na timu yao.

“Tumeshangazwa na taarifa za usajili wa Metacha na timu nyingine wakati wanafahamu ni mchezaji wetu halali kwasababu aliingia mkataba na sisi wa miaka miwili, ametumikia msimu mmoja bado mmoja,” alisema na kuongeza;

“Tunatarajia kuingia kambini kuanzia Agosti 17 hadi 20 ndani ya tarehe hizo tunatarajia pia kumwona Metacha akiungana na timu yetu kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi, hivyo sina mengi zaidi ya kuzungumza kwa sababu mkataba upo.”

Akizungumzia maandalizi ya msimu mpya alisema kwa sasa wanaendelea kufanya usajili na kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu.

Mkurugenzi wa ufundi wa SBS, Muhibu Kanu alifafanua juu ya mchezaji huyo waliyemsajili kuwa kwa mujibu wa mchezaji aliwathibitishia kuwa ni mchezaji huru ndio maana walifanya naye makubaliano.

“Tumesikia taarifa za Polisi Tanzania kuthibitisha kuwa bado wana mkataba na Metacha sio jambo jema walilolifanya kwenda moja kwa moja kwenye vyombo vya habari sheria zipo wazi wangefuata utaratibu,” alisema na kuongeza;

“Tunawaheshimu Polisi Tanzania kama kweli wana mkataba na Metacha tunawakaribisha mezani tulijadili hilo ili tusifike mbali zaidi na sio kufanya walichokifanya, jambo ambalo linaweza kutatuliwa kisheria au kulimaliza mezani sisi ni wamoja hatuwezi kugombea fito moja wakati tunalijenga soka letu lifike mbali,” alisema Kanu.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...VITA VYA MATAJIRI SOKA LA BONGO KUTAWALA...MWENYE NGUVU ZAIDI NDIYE BINGWA...