Home Habari za michezo PAMOJA NA KUSHINDA TUZO YA GOLI BORA….BAO LA SAKHO LAWEKA REKODI HII...

PAMOJA NA KUSHINDA TUZO YA GOLI BORA….BAO LA SAKHO LAWEKA REKODI HII KUBWA CAF…HAIJAWAHI TOKEA KAMWE…


Nyota wa Simba, Msenegal Pape Sakho amekuwa mchezaji wa kwanza anayecheza Ligi ndani ya Afrika Mashariki kushinda tuzo ya bao bora la msimu katika tuzo zinazoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF.

Katika tuzo hizo zilizofanyika Rabat, Moroccco usiku wa kuamkia leo bao Sakho alilofunga dhidi ya ASEC Mimosas kwa ‘tiktaka’ kwenye kombe la Shirikisho Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Februari 13 mwaka huu likiwa la kwanza katika ushindi wa 3-1 ilioupata Simba.

Bao hilo lilianzia kwa Peter Banda akipiga pasi fupi kwa Shomari Kapombe alipiga krosi ndefu na kuingia ndani ya boksi la ASEC ikamkuta Sakho na kufunga kwa tiktaka.

Katika kinyanga’anyiro hicho, bao la Sakho liliyashinda mabao mengine mawili ya Mmorocco Zouhair El Moutaraji wa Wydad Athletic ya Morocco na Mmalawi Gabadinho Mhango anayekipiga Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Sakho aliungana na Wasenegal wenzake kuisimamisha Afrika hapo jana kwani tuzo nyingi zilienda katika taifa hilo zikiwemo timu bora ya taifa, kocha bora (Aliou Cisse), Mchezaji bora wa Afrika anayecheza nje (Sadio Mane) na Mchezaji bora chipukizi iliyoenda kwa Pape Matar Sarr anayekipiga Tottenham ya England.

Klabu bora ilichaguliwa kuwa Mabingwa wa Afrika Wydad Casablanca ya Morocco na kipa wa Al Ahly, Mohamed El Shenawy aliibuka mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa

SOMA NA HII  YANGA ILIUA LIGI YA MUUNGANO...HIKI NDIO KILICHOTOKEA A-Z HADI KUSIMAMISHWA KWA KOMBE HILO