Home Habari za michezo SINGIDA BIG STARS HAWATANIII AISEE…WASHUSHA MASTAA WAPYA KUTOKA BRAZILI KIMYA KIMYA WALAH…

SINGIDA BIG STARS HAWATANIII AISEE…WASHUSHA MASTAA WAPYA KUTOKA BRAZILI KIMYA KIMYA WALAH…


Wamedhamiria, ndivyo unavyoweza kusema baada ya viongozi wa Singida Big Stars kupata saini ya Wabrazili, Bruno Gomez na Dario Fredrico.

Nyota hao licha ya kufichwa na timu hiyo ila taarifa ambazo zimetolewa ni kuwa wameanza mazoezi rasmi huku wakiwa chini ya uangalizi maalumu na baadhi ya viongozi hawataki wapigwe picha hadi watakapotambulishwa rasmi.

Gomes, Fredrico ni viungo washambuliaji wapo jijini Arusha kwenye kambi ya timu hiyo inayojiandaa na maandalizi ya msimu (pre season) na wameanza kuwavutia mabosi wao.

“Ni wachezaji wazuri na mazoezini wameonyesha wana vitu japokuwa viongozi wamefanya siri, ila muda wowote watawatambulisha akiwemo pia na Pascal (Wawa).” kilisema chanzo hicho.

Singida iliyo chini ya Mholanzi, Hans van der Pluijm na msaidizi wake Mganda, Mathias Lule inajifua jijini Arusha tangu Julai 22 na baada ya hapo itakwenda Singida ambako ndio makao yake makuu kujiandaa na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 17.

Hadi sasa Singida imenasa saini ya mastaa kadhaa wakiwemo, Aziz Andambwile (Mbeya City), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Benedict Haule (Azam FC) na Metacha Mnata (Polisi Tanzania). Wengine ni, Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Said Ndemla (Mtibwa Sugar), Pascal Wawa (Simba) na Deus Kaseke, Yassin Mustapha, Paul Godfrey ‘Boxer’ wote kutoka (Yanga).

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUTOKUTUMIKA KWENYE MECHI ZA CAF..HII HAPA SABABU YA SIMBA KUSAFIRI NA CHAMA LEO...