Home Habari za michezo SINGIDA BIG STARS WAONYESHA JEURI YA PESA….BAADA YA KUMRUDISHA KOCHA HANS PLUIJM…WAMVUTA...

SINGIDA BIG STARS WAONYESHA JEURI YA PESA….BAADA YA KUMRUDISHA KOCHA HANS PLUIJM…WAMVUTA NA PASCAL WAWA…


Beki wa kimataifa kutoka Ivory Coast aliyetemwa na Simba, Pascal Wawa amerejea nchini na kutua Singida Big Stars baada ya kocha wa timu hiyo, Hans Pluijm kumvuta ili aitumikie kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Wawa aliyeitumikia Simba kwa misimu minne tangu 2018 akitokea Al-Merrikh ya Sudan aliachana na timu hiyo Juni 23 mwaka huu kwa kuagwa kwa heshima katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Mtibwa Sugar.

Taarifa za kuaminika kutoka Singida Big Stars ilieleza nyota huyo kujiunga na timu hiyo, likiwa ni pendekezo la kocha Pluijm na msaidizi wake, Mathias Lule aliyekuwa akiifundisha Mbeya City. Baada ya Wawa kutua nchini usiku mwingi juzi alijiunga rasmi na timu hiyo moja kwa moja katika maandalizi yanayoendelea jijini Arusha.

Wawa ameungana na kina Aziz Andambwile, Kelvin Sabato, Metacha Mnata, Yassin Mustafa, Paul Godfrey ‘Boxer’, Benedict Haule, Abdulmajid Mangalo na Said Ndemla.

SOMA NA HII  KISA UCHAGUZI ...KADUGUDA ALIAMSHA SIMBA SC...AANIKA SAFARI YA BARBARA QATAR..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here