Home Habari za michezo SINGIDA BIS STARS WAZIDI KUTIKISA USAJILI BONGO…. WAPITA JUMLA JUMLA NA BEKI...

SINGIDA BIS STARS WAZIDI KUTIKISA USAJILI BONGO…. WAPITA JUMLA JUMLA NA BEKI KISIKI WA YANGA….


Klabu ya Singida Big Stars zamani (DTB) imeendelea kushusha vifaa vipya kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufanikiwa kupata saini ya aliyekuwa beki namba mbili wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu Yanga, Paul Godfrey ‘Boxer’.

Boxer amejiunga na timu hiyo ya ‘Wana alizeti’ kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia kushindwa kutamba kwa mabeki Djuma Shaban na Kibwana Shomari hali iliyomfanya kutafuta changamoto sehemu nyingine ili kunusuru kipaji chake.

Wageni hao wa Ligi Kuu Bara huo unakuwa ni usajili wa tatu hadi sasa baada ya kuwatambulisha mshambuliaji, Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza na kiungo Aziz Andambwile aliyesajiliwa kikosi hapo akitokea Mbeya City.

Usajili wa nyota huyo ni muendelezo wa kukisuka upya kikosi hicho kwani baadhi ya wachezaji waliofanikisha timu hiyo kupanda Ligi Kuu wako kwenye hatari ya kutwema hivyo uongozi umeanza maandalizi mapya kwa ajili ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 17.

SOMA NA HII  KISA TUHUMA ZA USHIRIKINA...MBRAZILI AINGILIA KATI BIFU LA KAPOMBE NA MWENDA...ISHU NZIMA IKO HIVI...