Habari za michezo

SAA KADHAA BAADA YA KUMALIZANA NA M-BET…TRY AGAIN AFUNGUKA HAYA KUHUSU TARIMBA WA SportPESA…

admin August 1, 2022 3:49 pm


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amemshukuru Mdhamini Mkuu aliyemaliza muda wake (SportPesa), kwa kufanikisha sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo kwa miaka mitano iliyopita.

‘Try Again’ ametoa shukurani hizo wakati akihutubia katika Hafla ya kutangaza thamani ya Mkataba Mpya wa klabu ya Simba SC na Kampuni ya Michezo ya Kubadhiri ya M-Bet iliyofanyika leo Jumatatu (Agosti Mosi), katika Hoteli ya Johari Rotana.

Try Again alisema: “Leo ni siku ya kuzungumza fedha. Kampuni kubwa hudhamini klabu kubwa.” “Sisi Simba ni waungwana, tunawashukuru wadhamini waliopita, sasa tuko na mdhamini mpya na tunaamini tutafanya kazi kwa karibu.”

“Tunakaribisha makampuni mengine kufanya nayo kazi sababu hii ni klabu ya watu, wasiogope tuko tayari kufanya nao kazi.”

“M-Bet mlichotaka mtakipata. Pesa ni nyingi hizi, tumieni hii nafasi kutanua biashara yenu kupitia mashabiki wetu.”

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo akagusia kwa uchache Siku ya Simba (Simba Day) iliyopangwa kufanyiaka Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Jumatatu (Agosti 08).

“Mimi sijawahi kuona Simba Day kama hii, imeandaliwa ikaandalika, naona kama siku haifiki. Tuje kwa wingi siku hiyo.”- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah (Try Again).

HIVI NDIVYO SIMBA WATAKAVYONUFAIKA NA MABILIONI YA M-BET…KILA MWAKA DAU LITAONGEZEKA MARA DUFU… KUHUSU ISHU YA AZAM KUMWAGANA NA MUDATHIRI YAHYA…UKWELI WOTE HUU HAPA…MAMBO NI KIMYA KIMYA AISEE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply