Habari za michezo

HUU HAPA UKWELI WA KAGERE KUSAJILIWA SINGIDA BIG STAR…PLUIJM NAYE NDANI YA NYUMBA….

admin August 4, 2022 12:06 pm


Taarifa za ndani kabisa zinaeleza kuwa, kuna uwezekano mkubwa leo Singida Big Star wakamtambulisha Meddie Kagere kuwa jembe lao jipya kwa ajili ya kuelekea kwenye mapambano ya Ligi Kuu 2022-23.

Imeelezwa kuwa, Singida Big Stars imeshakamilisha usajili na baada ya kusaini, amepewa ruksa ya siku kadhaa kurejea kwao Rwanda na kisha kurejea tena nchini kujiunga na matajiri hao wa Singida.

Akizungumza na Wasafi FM asubuhi ya leo, msemaji wa Singida Big Star, Dismas Ten, alisema wana sapraiz kubwa leo katika tamasha lao la kutambulisha wachezaji ambalo pia litahusisha mechi kati ya Singinda Big Star dhidi ya Zanaco ya Zambia.

“Tunayo sapraiz ambayo mashabiki wataiona hapo baadaye uwanjani. Kuhusu Kagere ni mchezaji mzuri, lakini ibaki kama nilivyokwambia sisi tunayo sapraiz hapo baadaye,” alisema Ten.

Kwenye ukurasa wao wa Instagram, Singida Big Star tayari wameweka picha za wachezaji wakiingia uwanjani na basi lao huku pia akionekana aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm ambaye amekula kandarasi ya kuwanoa matajiri hao wa Singida.

HAWA AZAM WAKO ‘SIRIAZI’ SANA AISEEE…HUKO MISRI WANAPIGA MATIZI YA KIULAYA ULAYA TU…WAMWAJIRI MWALIMU WA CHUO KIKUU.. NI MANARA TENA….SAFARI HII AJIREKODI VIDEO AKIMLILIA WAZIRI MCHENGERWA…AIANGUKIA SERIKALI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply