Habari za michezo

HUYU MAKAMBO SIO BUREE AISEEE…MAYELE ‘AKITIA NA YEYE ANATIA’ …..WOTE JANA’ WAMEITIA’ NAMUNGO MBILI ‘KAVUKAVU’….

admin August 4, 2022 2:47 am


Kikosi cha Yanga SC, kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC jana Jumatano, Agosti 3, 2022, Avic Town ambako wamekita kambi.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Fiston Mayele na Heritier Makambo na kuifanya safu ya ushambuliaji ya Yanga kutikisa nyavu mara 16 katika michezo mitatu ya kirafiki katika maandalizi yao ya kuelekea msimu mpya.

Akizungunzia mchezo huo, Kocha wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema ulikuwa mchezo mzuri na kipimo sahihi kwao kuelekea kuanza kwa ligi.

“Kabla ya mechi hii, tumecheza mechi nne na zote tumeshinda bao 4 kila mmchezo, lakini hiyo haikuwa kipimo sahihi, kwa Yanga tumejipima vizuri na kuona wapi yalipo mapungufu yetu.

“Kikosi chetu kina wachezaji wapya 15, na wote nimewaona uwezo wao ni mzuri, tunaamini watatupa tunachokitarajia katika msimu huu,” amesema Julio.

Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga walihitaji mechi tatu tu za kirafiki kujiandaa na msimu ambapo  wamekamilisha. Hivyo kwa sasa wanakwenda kujiandaa na mchezo wao Kilele cha Siku ya Wananchi, Agosti 6, kabla ya kuvaana na Simba kwenye Ngao ya Jamii, Agosti 13.

EPL IMERUDI TENA….YES ..NI KATIKA MSIMU WA SOKA LA KIBABE…FULHAM Vs LIVERPOOL…MZIGO WOTE HUU NDANI YA DStv…. KISA RATIBA YA LIGI KUU…KOCHA MKUU SIMBA AIBUKA HILI JIPYA…AVUNJA UKIMYA KUHUSU MECHI NYINGI ZA ‘HOME’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply