Habari za michezo

ACHANA NA STORI ZA KIJIWENI…SIMBA KUKIPIGA NA TIMU HII YENYE HADHI ZAIDI KWENYE MECHI YA SIMBA DAY MWAKA HUU..

admin August 5, 2022 7:00 am


Klabu ya Simba imethibitisha kucheza na St George katika kilele cha Siku ya Simba ‘Simba Day’ Agosti 8.

Nyota wa klabu hiyo kongwe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ethiopia, ndio mabingwa wa Ethiopia wakimaliza ligi hiyo kwa kukusanya jumla ya alama 65 mbele ya Fasil Kenema wenye alama 61. St. George FC watawasili nchini kesho Agosti 6, 2022.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema timu hiyo itawasili ikiwa na nyota wake wote tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Wapinzani wetu watawasili Dar es Salaam siku nne kabla ya kulele cha Simba day Agosti 8,” amesema.

Simba inafanya tamasha hilo kwa mara ya 14 msimu huu tangu lilipoanzishwa mwaka 2009, pamoja na shamra shamra nyingine, watalitumia kutambulisha wachezaji wao wapya kabla ya kucheza mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki.

KISA MANARA KUOMBA MSAMAHA KWA WAZIRI….JEMEDARI SAIDI AIBUKA NA KUMPA TENA ‘MAKAVU LIVE’… KISA KUSHIRIKI AFCON….KLABU YA NAPOLI YA ITALI WAKATAA KUSAJILI MCHEZAJI KUTOKA AFRIKA…WAPIGA MKWARA HASWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply