Habari za michezo

KISA MANARA KUOMBA MSAMAHA KWA WAZIRI….JEMEDARI SAIDI AIBUKA NA KUMPA TENA ‘MAKAVU LIVE’…

admin August 5, 2022 7:00 am


Jemedari Said Kazumari amekua ni moja ya watu wanaozungumzia kwa ukaribu sakata la manara na TFF kwa siku za karibuni, Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika andiko refu kuhusu haji kuomba radhi kwa waziri juu ya kauli aliyo itoa siku chache zilizopita

Kwenye andiko hilo Jemedari ameandika;

“Kumsaidia Haji ni kumuambia UKWELI pale anapokosea tu, wanaomzunguka HAWAMPENDI kwakuwa hawawezi kumuambia ukweli mchungu ambao ni tiba kwa tabia zake.”

“Tunaoonekana hatumpendi ndio kiuhalisia TUNAMPENDA ila kwakuwa anazungukwa na WAHUNI ambao wanamuelekeza shimoni na yeye kajivika upofu ndiyo maana ndani ya siku 3 anaomba msamaha mara 2.”

Ukimuambia ukweli wewe ni adui na WAPAMBE watakuandama sana kwa maneno, lakini leo masikini ya Mungu anahangaika pekeyake na misamaha isiyoisha.

Kwa kuongezea Jemedari saidi amesema Haji HACHUKIWI ingawa yeye mwenyewe hajipendi na wanaomzunguka hawajahi kumpenda.

Wanashangilia anguko lake kwa kumvika Ufalme hewa na yeye anajiona mfalme kweli kumbe anajiingiza kwenye lindi la matatizo.

Tunaomuambia ukweli ni vile tunaochukizwa na tabia zake ambazo sio za kiuanamichezo anazozionyesha kila uchao kwa watu tofauti tofauti.

Nakukumbusha tu kumuomba msamaha Waziri na ukakiri kukosea hadharani ni vyema sana. Lakini pia unadhihirisha kwamba ulipomkosea Waziri ulifanya kosa la KIMAADILI.

Kosa la kimaadili linaweza kuishi hata miaka 10 likafufuliwa na ukashitakiwa nalo na ukaadhibiwa. Wanaokuchukia hawawezi kukuambia hivi. Sisi tunaokupenda pekee ndo tunakupa ukumbusho huu jadidi.

BAADA YA TIMU ZA TZ KUMSHINDWA ….IBENGE APATA SHAVU NONO LA KUINOA AL HILAL…APEWA MALENGO KAMA YA SIMBA… ACHANA NA STORI ZA KIJIWENI…SIMBA KUKIPIGA NA TIMU HII YENYE HADHI ZAIDI KWENYE MECHI YA SIMBA DAY MWAKA HUU..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply