Habari za michezo

KIULAINIII….NABI AFUNGA MACHO NA KUSAINI MKATABA MPYA YANGA….AKATAA MAMILIONI YA WAARABU…

admin August 5, 2022 5:00 pm


Klabu ya Soka ya Yanga imethibitisha kocha wake Nasredin Mohammed Nabi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia timu hiyo ya ‘Wananchi’ hadi mwaka 2024.

Licha ya Nabi kuhitaji ongezo zaidi la mshahara ambao wameafikiana, kingine ni mipango yake ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania.

Kila Kocha anapenda kufanikiwa na timu anayofundisha hata kama haipendi. Nabi anaamini anaweza kupata mafanikio aliyokosa alikopita, kama Yanga wanavyoamini pia juu yake hasa kufuatia kuimarishwa kwa kila idara ndani ya kikosi hicho msimu huu.

Nabi ameiongoza Yanga kutwaa mataji matatu mhimu msimu uliyopita baada ya Yanga kuwa na ukame wa makombe kwa miaka minne.

Baada ya kusaini kandarasi hiyo, Nabi amesema; “Bado nipo nipo sana, Safi fresh.”

KUELEKEA MECHI YA NGAO YA JAMII…SIMBA WAANDAA SILAHA ZA SIRI KUIMALIZA YANGA…UKWELI WOTE HUU HAPA… KUELEKEA SIKU YA WANANCHI…YANGA HAWATAKI DENI AISEEE…WAALIZANA KIMYA KIMYA NA MAYELE…DILI LA SAUZI LAFAA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply