Habari za michezo

MANARA ALIPOGEUZA SIKU YA WANANCHI JANA KUWA FURSA KWAKE…AJIPA ‘UMC’ WA MITAANI…KITENGE AKAZIA YA TFF…

admin August 7, 2022 3:29 am


Haji Manara msemaji wa Yanga anayetumikia  kifungo cha kukaa nje miaka miwili, alichoadhibiwa na kamati ya utendaji ya  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ametoa ufafanuzi wa kwa nini ametambulisha wachezaji wa timu hiyo.

Manara baada ya kumaliza kazi ya kutambulisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, amesema kazi hiyo kama  MC mwalikwa na ahusiki na mambo ya soka kabisa.

Adhabu ya Manara aliyopewa na kamati  ya nidhamu ya TFF, inamtaka asijihusishe na kitu chochote kinachohusiana na michezo.

Manara amesema “Nipo hapa kama walivyoalikwa kina Zembwela, Dakota na Maulid Kitenge, nimemaliza kazi yangu naondoka kabisa uwanjani kwenda kwenye kazi ya UMC Kidogo.”

Alidakia Kitenge aliyesema “Tena ni MC tuliyemtoa Manzese mtaani, hivyo ahusiani na mambo ya soka.”

Manara ni kama ametoa ufafanuzi kwa mashabiki waliyokuwa wakijiuliza kwa inakuaje Manara anatambulisha wachezaji wakati ana adhabu.

BAADA YA KUBANJULIWA 2-0 JANA….NABI BILA KUPEPESA MACHO AANIKA MADHAIFU YA YANGA…”WACHEZAJI WALIFANYA MAKOSA”…. BAADA YA KUONA ‘BYUTI BYUTI’ YA YANGA ….’TRY AGAIN’ KATIKISA KICHWA WEEEH..KISHA AKASEMA HAYA KUHUSU SIMBA DAY…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply