Azam FC

KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA….GEITA GOLD WAPEWA MIFUPA MIGUMU TUPU…AZAM WAPEWA WAARABU WEUSI TUPU…

admin August 9, 2022 5:45 pm


Matajiri wa madini, Klabu ya Geita Gold imepangwa kukutana na timu ya Hilal Al Sahil ya Sudan Kaskazini katika mechi ya hatua ya awali raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Katika raundi ya pili ya mtoano, mshindi kati ya Geita Gold na Hilal Al Sahil atakutana na Pyramids FC ya Misri.

Matajiri wa jiji la Dar, Azam FC ambao wanaanzia katika hatua ya pili ya mtoano katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, wamepangwa kukutana na mshindi kati ya Al Akhder ya Libya na Al Ahli Khartoum ya Sudan Kaskazini.

Al Akhder na Al Ahli Khartoum watakipiga katika raundi ya kwanza ya mtoano ambapo mshindi kati yao ndiye atakutana na Azam katika hatua inayofuata.

Mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 9, 10 na 11, mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 16, 17 na 18 mwaka huu.

Adha, michezo ya kwanza raundi ya pili ya mtoano itapigwa Oktoba 7, 8 na 9 mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano za raundi ya pili ya mtoano zitapigwa Oktoba 14, 14 na 16, mwaka huu.

LIGI YA MABINGWA AFRIKA…SIMBA WAPELEKWA MALAWI…YANGA WAPEWA WASUDANI KUSIN…MECHO ZOTE KUPIWA HIVI… MICHUANO YA CAF…KAZI IPO KWA TIMU ZA TANZANIA…OKWA  AZIDI KUTAMBA NA ‘KAGOLI’ KAKE KAMOJA…NABI ARINGA NA AZIZ KI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply