Baada ya mechi dhidi ya St George ya Ethiopia katika Simba Day Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alifurahishwa na umati uliojitokeza kukiona kikosi huku akiwaambia anadhani wameona usajili wao.
โAsanteni kwa kuitikia wito kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha kubwa. Wachezaji mmewaona nawaomba mje kwa wingi Jumamosi kuona soka la ushindani, tumefanya usajili bora,โ alisema.
โMatokeo tuliyoyapata yanaongeza chachu ya ushindani hadi kufikia Jumamosi tunatarajia mambo mazuri zaidi.โ