Habari za michezo

BAADA YA BUMBULI KUONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA YANGA….KATI YA HAWA WANNE MMOJA WAO KUMRITHI…

admin August 12, 2022 6:00 pm


Siku moja baada ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick kukiri kuwa wameachana na aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Hassan Bumbuli tayari tetesi zimezagaa kuhusu mrithi wa Nafasi hiyo..

Wakili Simon akihojiwa na kituo cha Uhai FM alikiri kuwa wameachana na Bumbuli baada ya Mkataba wake kumalizika na hivyo nafasi hiyo kwa sasa ipo wazi kwa yeyote mwenye vigezo anaruhusiwa kutuma maombi.

Sasa tayari kundi la wanahabari vijana wanatajwa kutuma maombi kutaka nafasi hiyo ambao ni Ali Kamwe, Juma Ayo (amekiri kutuma maombi), Ahmed Abdallah na mwanadada Prisca Kishamba.

Katika Majina hayo ambayo yameshatuma maombi mpaka wakati huu jina la Mwandishi wa habari za michezo kutoka kituo cha Azam Media Ali Kamwe linapewa kipaumbele kuchukua nafasi hiyo.

FIFA KUUMULIKA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KESHO….MWAMUZI WAO AKABIDHIWA RUNGU… NABI ANADAWA YA OKRAH NA SAKHO…ATAMBA KAZI INAISHA ASUBUHI TU…CHAMA OKWA TISHIO KWA YANGA LEO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply