Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewaonya Mashabiki wa Soka watakaokwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya Mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi (Agosti 13).
Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans watapapatuana na Simba SC katika mchezo huo ambao utatumika kama kiashirio cha ufunguzi wa Msimu Mpya 2022/23.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne Muliro amezungumza na Waandishi wa Habari na kusema, shabiki yoyote hataruhusiwa kwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa akiwa na silaha isipokuwa vyombo vya dola.
โKatika kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam litachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo, usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juuโ
โNi marufuku kwa Mtu yeyote kwenda na silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo, tunawatoa hofu Mashabiki watakaofika kushuhudia mchezo huo kuwa ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa umeimarishwa kwa kiwango cha juuโ amesema Kamanda Muriro