Habari za michezo

RASMI…YANGA WATHIBITISHA KUACHANA NA BUMBULI….HUYU HAPA MTANGAZAJI WA AZAM TV ANAYETAJWA KUMRITHI…

admin August 12, 2022 9:21 am


Uongozi wa klabu ya Yanga, kupitia kwa Kaimu Mtendaji wake Mkuu, Simon Patrick umethibitisha kuachana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli.

Kwa mantiki hiyo sasa, nafasi hiyo iko Wazi na wenye Sifa wanaruhusiwa kutuma maombi.

Kuachana kwa Bumbuli na Klabu ya Yanga, ni kukamilisha tetesi zilizoanza kuvuma siku chache zilizopita kuwa BUmbuli ametemwa klabuni hapo.

Pamoja na Mshereheshaji maarufu nchini Taji Liundi kukaimu nafasi ya Bumbuli wakati wa maandalizi ya Siku ya Wananchi, Mchambuzi na mtangazaji wa Azam TV, Ally Kamwe anatajwa kuwa miongoni mwa watu watakaopewa nafasi hiyo.

Bumbuli ni miongoni mwa waliokuwa waajiriwa wa Yanga wakati wa utawala wa Dk Mshindo Msola ambapo mara baada ya kuingia utawala mpya wa Injinia Hersi Saidi, mabadiliko mengi yalifanyika ikiwemo aliyekuwa Mtendaji Mkuu Senzo Mbatta ambaye aliondoka mara baada ya mkataba wake kuisha.

KISA YANGA vs SIMBA KESHO…OKRAH ATAMBA HIZI NDIO MECHI ZAKE…MASTAA YANGA WAPIKIWA MSOSI MAALUMU KAMBINI… BAADA YA KUONA MASHABIKI WA YANGA WAMEPOA KUELEKEA MECHI YA KESHO….NABI AIBUKA NA HILI KUHUSU AZIZ KI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply