Home Habari za michezo KUFUZU LIGI YA MABINGWA KWA WANAWAKE AFRIKA….SIMBA QUEENS WAINGIA UBARIDI GHAFLA…WATISHWA NA...

KUFUZU LIGI YA MABINGWA KWA WANAWAKE AFRIKA….SIMBA QUEENS WAINGIA UBARIDI GHAFLA…WATISHWA NA WAETHIOPIA…


Nahodha wa timu ya wanawake ya Commercial Bank of Ethiopia (CBE), Loza Abera ametamba kuwa timu yake imejipanga kuhakikisha inatwaa ubingwa wa mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yatakayoanza keshokutwa Jumapili ambao utawapa tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake.

Mashindano hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam yakishirikisha jumla ya timu nane huku Simba Queens ya Tanzania ikiwa ni miongoni mwa timu shiriki.

Mwaka jana, timu hiyo ya CBE ilitinga hatua ya fainali ya mashindano hayo ya kufuzu Ligi yaMabingwa Afrika kwa Wanawake kwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati na kupoteza mbele ya Vihiga Queens ya Kenya kwa mabao 2-1.

Akizungumzia mashindano ya mwaka huu, Abela alisema watafanya zaidi ya pale walipoishia kwa kutwaa ubingwa ili waweze kushiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

“Baada ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita, tuko tayari kuhakikisha tunafanya vizuri na kutwaa taji mwaka huu. Timu ina hamasa na imejiandaa kuchukua ubingwa na kupata tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa Afrika,” alisema Abela.

Msafara wa wachezaji 20 wa CBE uliwasili Tanzania juzi tayari kwa kushiriki mashindano hayo.

Wachezaji wanaounda kikosi cha CBE ambao watashiriki mashindano hayo ni Tarikua Bergena, Negesti Meaz, Hasabe Muez, Tizta Haile Michael, Etsegenet Bezuneh, Bezuayehu Tadesse, Teruanchi Mengesha, Nardos Getnet, Berke Amare, Embet Addisu, Bertukan Gebre Kirstos, Senayet Bogale, Tigist Yadeta, Tarikua Debeso, Mesay Temsegen, Loza Abera, Medina Awol, Tseganesh Worena, Aregash Kalsa na Ariat Odong

SOMA NA HII  KOMBE LA DUNIA NA MACHAGUO SPESHO MERIDIANBET TWEN'ZETU KIBINGWA QATAR....