Habari za michezo

BAADA YA UKIMYA MWIINGII….HATIMAYE ZAHERA AVUNJA UKIMYA YANGA…ATAJA TATIZO LA SOKA LA TZ

admin August 13, 2022 12:24 pm

 


MKURUGENZI wa Ufundi wa Yanga, Mwinyi Zahera, amezitaka klabu zote hapa nchini kutengeneza wachezaji vijana kwa ajili ya kuwaandaa kuwa wanasoka nyota wa baadaye na si kubakia katika vita ya kushinda vikombe pekee.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Zahera, alisema amekuwa akiwatengeneza wachezaji vijana chini ya miaka 17 na miaka 20 kwa ajili ya kuwabadilisha na kuwa wachezaji wenye uwezo na maarifa makubwa.

“Soka la vijana ni kama shule, huko kuna wa kwanza hadi wa mwisho huku walimu wakiangalia namna ya kuwaendeleza wale walio juu na kuwarekebisha waliko chini ili nao viwango vyao vipande.

“Hakuna klabu ambayo inatengeneza wachezaji wa umri chini ya miaka 17 na miaka 20 wote waje kuwa nyota, ndiyo maana unaona timu nyingi kubwa duniani zina wachezaji vijana, lakini si wote wanaokwenda kuchezea timu kubwa au kuwa nyota,” alisema Zahera.

Aliongeza naye anawatengeneza wachezaji katika klabu hiyo kwa mfumo huo na anazikumbusha timu nyingine kufuata nyayo hizo badala ya kujipanga  kushinda mataji pekee.

“Na hata mazoezi ninayowapa, hatufanyi kwa ajili ya kuchukua ubingwa, ni yale ya kuwajenga watoto na kuwapata hata wawili watatu ambao wanaweza kwenda timu kubwa, hiyo falsafa ya mafunzo kwa wachezaji vijana duniani kote,” alisema Mkongomani huyo.

KUFUZU LIGI YA MABINGWA KWA WANAWAKE AFRIKA….SIMBA QUEENS WAINGIA UBARIDI GHAFLA…WATISHWA NA WAETHIOPIA… ACHANA NA STORI ZA KUSIKIA…HUU HAPA UKWELI WOTE KUHUSU MASHINDANO MAPYA YA CAF SUPER LEAGUE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply