Habari za michezo

BAADA YA KUBANJULIWA NA YANGA JUZI….MAKI APUKUTISHA MIKONO SIMBA…ATOA TAHADHARI KWA TIMU ZA LIGI KUU…

admin August 16, 2022 9:17 am


BAADA ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 2-1 Simba,kete ya kwanza kwa Kocha Mkuu,Zoran Maki kwenye ligi ni dhidi ya Geita Gold,utakaochezwa Jumatano, Uwanja wa Mkapa.

Maki ana kibarua cha kuweza kuanza kusaka taji la Ligi Kuu Bara ambalo lipo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu,Nassredine Nabi.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba wanatambua kazi ambayo ipo kwenye ligi ni kubwa na wachezaji wanalitambua jambo hilo.

“Tumeshindwa kupata taji la Ngao ya Jamii baada ya kupoteza mchezo wetu dhidi ya Yanga tunatambua kwamba tulikuwa tunahitaji ushindi lakini haijawa hivyo.

“Kwa mechi ambazo zinakuja hasa kwenye ligi yale makosa ambayo tumefanya ni muhimu kwetu kuweza kuyafanyia kazi ili kupata ushindi,” amesema.

Ndani ya Geita Gold yupo mshambuliaji namba moja kwa utupiaji ambaye ni George Mpole aliyekamilisha msimu wa 2021/22 kwa kutupia mabao 17.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa,Simba ilishinda mabao 2-1 ambapo watupiaji kwa Simba ilikuwa ni Peter Banda na Mzamiru Yassin.

Moja ya bao aliweza kuwatungua Simba walipokutana kwenye mchezo wa ligi msimu uliopita walipogawana pointi mojamoja.

ZILE KUKURU KAKARA ZA LIGI KUU YA NBC ZINAENDELEA TENA LEO….RATIBA NZIMA HII HAPA…UHONDO WOTE NDANI YA AZAM TV… KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA POLISI TZ….NABI AJIPALILIA MAKAA…MASTAA YANGA WAKAA MGUU PANDE KULIWASHA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply