BIashara United

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA POLISI TZ….NABI AJIPALILIA MAKAA…MASTAA YANGA WAKAA MGUU PANDE KULIWASHA…

admin August 16, 2022 9:23 am


BAADA ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba,Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi leo Agosti 16 inafungua ukurasa kwenye Ligi Kuu Bara kwa kusaka ushindi mbele ya Polisi Tanzania.

Yanga waliweza kutetea taji lao la kwanza ambalo walitwaa msimu uliopita wa 2021/22 ambapo walitwaa taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.

Mtupiaji kwa msimu wa 2021/22 alikuwa ni Fiston Mayele ambaye msimu huu wa 2022/23 amewatungua kwa mara nyingine Simba Uwanja wa Mkapa mabao yote mawili na kuipa taji la kwanza Yanga.

Nabi ameweka wazi kwamba anatambua mchezo utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya kuweza kupata matokeo.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tunahitaji kupata pointi tatu muhimu,timu ambayo tunakutana nayo ni imara hivyo nasi tuna kazi ya kufanya hilo lipo wazi”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo na timu Arusha ni pamoja na Fiston Mayele,Bernard Morrison,Aziz KI na Aboutwalib Mshery.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo majira ya 10:00 jioni.

BAADA YA KUBANJULIWA NA YANGA JUZI….MAKI APUKUTISHA MIKONO SIMBA…ATOA TAHADHARI KWA TIMU ZA LIGI KUU… MPOLE AISUSA GEITA GOLD….AGOMA KUJIUNGA NA TIMU MPAKA KIELEWEKE KWANZA…UONGOZI WATOA TAMKO HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply