Home Habari za michezo PAMOJA NA KUONDOLEWA MSIMBAZI…ADEL ZRANE ANDELEA KUIZUNGUMZIA SIMBA KWA STAILI HII…ATOA DUKUDUKU...

PAMOJA NA KUONDOLEWA MSIMBAZI…ADEL ZRANE ANDELEA KUIZUNGUMZIA SIMBA KWA STAILI HII…ATOA DUKUDUKU LAKE…

Aliyekua Kocha wa Viungo wa Simba SC Adel Zrane ameitabiria mema klabu hiyo msimu huu 2022/23, baada ya kuifuatilia katika michezo miwili iliyopita.

Simba SC iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mabingwa wa Ethiopia St George katika Tamasha la Simba Day Jumatatu (Agosti 08) na Jumamosi (Agosti 13) ilicheza dhidi ya Young Africans kuwania Ngao ya Jamii.

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba SC kupoteza kwa 2-1, matokeo ambayo yaliibua taharuki kwa mashabiki wengi wa soka ambao walikua wakihoji uwezo wa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.

Zrane ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye klabu ya Wehdat ya Jordan amesema amewatazama vizuri Simba SC na kugudua wana kikosi bora kulinganisha na msimu uliopita, ila wanahitaji muda tu kurejea katika makali yao.

“Nilikua sehemu ya watu ambao walipata nafasi ya kuangalia mchezo wa dabi siku ya Jumamosi, naweza kusema ulikuwa mchezo mzuri na wa ushindani, nilichogungua ni kuwa Simba SC hii ni bora zaidi kuliko ya msimu uliopita.

“Walicheza vizuri na kutokana na maingizo mengi mapya naamini kama watapata muda zaidi wa kuendelea kuwa pamoja, basi watafanya vizuri msimu huu kulinganisha na msimu uliopita ambao walikuwa na wakati mbaya sana.” amesema Zrane

Simba SC ilianza Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana Jumatano (Agosti 17) kwa kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Geita Gold FC, mabao yalifungwa na Augustine Okrah, Moses Phiri na Clatous Chama.

SOMA NA HII  GOMES - MATOKEO YA JUMAMOSI YAMETUUMIZA MNO