Habari za michezo

SHABIKI BILIONEA WA MAN UTD ASHINDWA KUVUMILIA VIPIGO…AAMUA KUWEKA MZIGO KUINUNUA KLABU HIYO…

admin August 18, 2022 6:15 pm


Bilionea Sir Jim Ratcliffe, ambaye anamiliki timu ya waendesha Baiskeli Ineos Grenadiers, yuko tayari kuinunua Manchester United na wachezaji wa zamani watahusishwa pamoja na Meneja Mkuu wa Grenadiers Sir Dave Brailsford.

Bilionea huyo wa Uingereza, ambaye ana utajiri wa dola Bilioni 7.18, kulingana na Bloomberg, hakufanikiwa katika ombi lake la dakika za mwisho la Euro Bilioni 4.25 kuinunua Chelsea mwezi Mei mwaka huu, huku mfanyabiashara Mmarekani Todd Boehly akifanikiwa kuipata klabu hiyo, na Ratcliffe sasa ameelekeza mawazo yake kwa Mashetani Wekundu.

Nia yake inakuja baada ya ripoti ya Bloomberg kusema kwamba familia ya Glazer ambao wamemiliki United tangu 2005, wanafikiria kuuza hisa chache katika klabu hiyo.

Majadiliano ya awali yamefanyika kuhusu kuleta mwekezaji mpya, kulingana na taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la Sky Sports, ambalo linamtaja Bilionea Ratcliffe kama mtu tajiri wa sita nchini Uingereza.

Msemaji wa Ineos alisema kampuni hiyo ingependelea kununua hisa ndogo kwa nia ya kuja kuinunua klabu hiyo kabisa.

USHINDI WA GOLI 3-0 DHIDI YA GEITA WAMRUDISHA MJINI AHMED ALLY…AANZA TAMBO NA MADONGO KWA YANGA TENA… SIMBA HAWAJAMALIZA KWELI….WAVUTA MIDO MNIGERIA…AKPAN HATIHATI, MUDATHIR ANUKIA MSIMBAZI…MAYELE ANAYAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply