Habari za michezo

HAWA WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA NAO SI HABA AISEE…WAPATA ‘KOCHA LA MBINU ZA USHINDI’…ALIKUWA AL HILAL..

admin August 21, 2022 10:29 am


Wapinzani wa Yanga kwenye hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, Zalan FC ya Sudan ya Kusini juzi wamemtambulisha kocha mpya Baping Alliab.

Alliab ambaye amewahi kuwa Kocha wa Al Hilal Wau Sudan Kusini na kubeba Kombe la Ligi ataiongoza Zalan kwenye mechi za Afrika ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Septemba 9 hadi 11 huku marudiano ikichezwa Septemba 16 mpaka 18.

Mshindi wa jumla baina ya klabu hizo atacheza na mshindi kati ya St.Georges ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

“Uongozi wa Zalan FC unathibitisha kumteua Baping Aliap kama kocha mkuu wa Zalan FC kwa kipindi cha mwaka mmoja (1) ikitegemea kumuongeza mkataba kutokana na kiwango timu itakachoonyesha,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Kocha huyo msimu uliopita alikuwa anakinoa kikosi cha Al Hilal Wau ambapo waliibuka Mabingwa wa Sudan Kusini.

YANGA WAZIDI KULISHIKA SOKA LA BONGO KIVYAO VYAO….USHINDI DHIDI YA COASTA JANA WAIPA REKODI HII YA KUDUMU…. HIVI NDIVYO ‘TAMBO NA MANENO YA SHOMBO’ YANAVYOMPA ULAJI MANDONGA MTU KAZI…LEO KUZICHAPA NA BONDIA HUYU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply