Habari za michezo

HIVI NDIVYO WASUDAN ZALAN FC WALIVYOIPA YANGA ‘KAMTELEZO’ KA KUFUZU MAKUNDI ….CAF WABARIKI MIPANGO YAO ….

admin August 23, 2022 12:42 pm


Klabu ya Zalan ya Sudan Kusini imewasilisha rasmi maombi ya mechi zao zote dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Yanga zichezwe hapa nchini kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zilizothibitishwa na uongozi wa klabu hiyo ni kwamba wapinzani hao wamewasilisha maombi hayo kuwa mechi zao mbili za hatua ya awali za Ligi ya Mabingwa Afrika zichizwe hapa nchini kama ambavyo kalenda ya mashindano ya CAF inavyoonyesha.

Tayari Zalan wameshakubaliwa maombi yao hayo huku wakitaja sababu ya viwanja vyao kukosa ubora wa kutumnika katika mashindano ya CAF kuwa ndio sababu kubwa.

Zalan ilitakiwa kuanzia kucheza nyumbani kati ya Septemba 9-11 mchezo ambao sasa utapigwa hapa nchini kisha timu hizo kurudiana tena baada ya wiki moja hapohapo Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Hiyo inakuwa mteremko zaidi kwa Yanga ambao hawatatumia gharama kubwa walizotakiwa kutumia kuisafirisha timu yao wakibakiwa na kazi moja tu kuwatupa nje ya masahindano Wasudan hao.

Endapo Yanga itafuzu hatua hiyo itakutana na mshindi kati ya St George ya Ethiopia watakaokutana na matajiri wa Sudan Al Hilal.

BAADA YA KUTOMCHEZA KWA MICHEZO YOTE MPAKA SASA…KOCHA SIMBA AIBUKA NA HILI KUHUSU HATMA YA BOCCO…. STAA WA AZAM AULA UTEUZI TAIFA STRAS…NI BAADA YA KUFUNGA GOLI LA KIDEONI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply