Habari za michezo

KOCHA MAKI AWAUMBUA WALIOKUWA WAKIMBEZA STRAIKA ‘MZUNGU’….AWATAKA WATULIE KAMA MAJI KWENYE NDOOO…

admin August 23, 2022 12:00 pm


KOCHA wa Simba, Zoran Maki, amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasiwe na haraka na uwezo wa mshambuliaji wa timu hiyo, Dejan Georgejevic, kwani tayari ameshaanza kuwaonyesha ubora wake wa kufunga ndani ya timu hiyo.

Dejan ambaye ni ingizo jipya, tayari amefanikiwa kufungua akaunti ya mabao ndani ya Simba mara baada ya kufunga bao katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo Simba walicheza dhidi ya Kagera Sugar.

kocha Maki alisema kuwa kwa wale wote ambao walikuwa wanahoji ubora na uwezo wa Dejan wanatakiwa kutulia kwani tayari wamejionea uwezo wake na ni jambo la subira kwa mchezaji mpya katika timu yoyote kuanza kwa kufanya vizuri.

“Wanatakiwa kuangalia kuifutilia timu kwa ukaribu lakini kuhusu Dejan labda huko mbeleni ndio walitakiwa kuhoji kuhusu ubora wake na sio kwa sasa kwani ni mapema mno kwa mchezaji mpya ndani ya timu.

“Lakini pia watakuwa wamejionea uwezo wake wa kufunga kupitia mchezo dhidi ya Kagera, kila kitu kitakuwa sawa, sio pekee tu kuna wachezaji wengine wengi tunaamini watakuja kutusaidia sana huko mbeleni na sio mapema hii na huo ndio mpira,” alisema kocha huyo.

AZIZ KI AFUNGUKA MAZITO …ATAJA MZIGO ALIOPEWA NA YANGA MSIMU HUU…SIMBA NA KIUNGO MNIGERIA MAMBO YAKO HIVI.. WAKATI PICHA ZA MANZOKI AKIWA UWANJA WA NDEGE KWA SAFARI ZIKISAMBAA ….NABI AENDELEA KUSISITIZA JINA LAKE YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply