Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA KUTEMWA SIMBA….KAPAMA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z KUTOONEKANA KAMBINI…

admin August 23, 2022 3:54 pm


Kiungo wa Simba, Nassoro Kapama hakuwepo katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Jumapili asubuhi siku moja baada ya kikosi hicho kutoka kucheza mechi dhidi ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kumekuwa na taarifa nyingi za kuhusu kiungo huyo kuondoka Simba kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha timu hiyo tangu kimerejea nchini kutokea Misri.

Alipoulizwa Kapama amesema alishindwa kwenda mazoezi kutokana na sababu za kifamilia zilizokuwa nje ya uwezo wake hadi kushindwa kuwepo katika awamu hiyo moja ya mazoezi.

Kapama amesema hakuna suala lolote kuhusu kuondoka Simba na hayo masuala mengine ni mambo ya kifamilia ambayo yanaendelea katika mitandao ya kijamii.

“Nipo kwenye timu na naendelea ratiba zote za timu kama ilivyo kawaida nilishindwa kuwepo kutokana katika mazoezi kutokana na mambo hayo ya kifamilia yakimalizika nitakuwepo kama kawaida,” amesema Kapama.

STAA WA AZAM AULA UTEUZI TAIFA STRAS…NI BAADA YA KUFUNGA GOLI LA KIDEONI… PAMOJA NA KUCHEZA MECHI MBILI TU….ZAHERA KAITAZAMA YANGA WEEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply