Home Azam FC PAMOJA NA UWEPO WA MASTAA WAKUBWA ….DUBE APITISHWA AZAM FC…KOCHA MSOMALI AMPA...

PAMOJA NA UWEPO WA MASTAA WAKUBWA ….DUBE APITISHWA AZAM FC…KOCHA MSOMALI AMPA MBELEKO ….


Kocha wa Azam, Abdihamid Moallin anatarajia kufanya mabadiliko kwenye kikosi katika michezo ijayo.

Moallin alisema moja ya mabadiliko hayo ni eneo la ushambuliaji ambalo kwa mechi mbili za Ligi Kuu Bara ameanza na Prince Dube pekee.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, alisema licha ya kuanza na mshambuliaji mmoja ila anafikiria kuwachezesha wawili ingawa haitakuwa rahisi kwani itategemea na ubora wa mpinzani wanayekutana.

“Chaguo langu kwa sasa ni Prince Dube ila huko mbeleni anaweza akaanza pamoja na Idris Mbombo au Rodgers Kola kwani itategemea na ubora wa mpinzani wetu, ingawa bado ni mapema sana,” alisema Moallin.

“Jambo linalonipa faraja ni uwepo wa kikosi bora kwenye kila maeneo, kila mchezaji ameonyesha utayari na ari ya kuipambania timu hii ni silaha kubwa kwetu katika kutimiza malengo tuliyojiwekea kwa msimu huu,” alisema.

Kauli ya Moallin imekuja baada ya Mbombo (Idris) na Rodgers (Kola) kuanzia benchi michezo miwili ya mwanzo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold licha ya msimu uliopita kuonyesha kiwango bora.

Kikosi hicho kinatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Djibout, AS Arta Solar 7, mechi itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex Agosti 30.

SOMA NA HII  NABI:- AZIZ KI HAKUCHEZA KWA MASLAHI YA YANGA...HAKUWA BORA KWANGU ...