Habari za michezo

UNAAMBIWA SIO ONYANGO TU….SADIO KANUOTE NAYE HAJAENDA NA TIMU SUDANI….YEYE KAAMUA KWENDA KWAO KABISA…

admin August 27, 2022 2:41 pm


SADIO Kanoute, kiungo wa kazi ngumu ndani ya Simba hayupo na timu nchini Sudan kutokana na kupewa ruhusa maalumu kuelekea nchini Mali kushughulikia pasi yake ya kusafiria.

Simba imeweka kambi kwa muda nchini Sudan ambapo wamealikwa kwenye mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Klabu ya Al Hilal.

Anatarajiwa kukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko na ule dhidi ya Al Hilal baada ya kupewa ruhusa na uongozi.

Ikumbukwe kwamba kikosi cha Simba kilikwea pipa Alhamisi na kuibukia nchini Sudan kikiwa na msafara wa wachezaji 19 ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Sadio Kanoute, Peter Banda na Vicctor Ackpan.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kiungo huyo hayupo kwenye kikosi ambacho kimekwenda Sudan.

“Ni kweli kiungo wetu Sadio Kanoute hayupo kwenye sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimesafiri kuelekea Sudan kwa ajili mashindano ambayo yameandaliwa na Al Hilal kutokana na kupewa ruhusa ili ashughulikie pasi yake ya kusafiria,”.

BAADA YA KUMALIZA MECHI ZA AWALI ZA MIKOANI….NABI KAVUTA KITI NA KUJIPONGEZA NA MAJI BARIDII…LAKINI AKASEMA HAYA… BAADA YA KUTOA GUNDU KWA KUIFUNGA LIVER JUZI…MAN UTD WAZIDI KUTAKATA EPL…RONALDO APEWA MECHI YA MWISHO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply