Habari za michezo

HII HAPA NJIA YA MAYELE KUIBUKA MFUNGAJI BORA AFRIKA…MECHI MBILI TU ANABEBA KIATU CHA DHAHABU….

admin August 30, 2022 2:54 pm


Mayele akizichanga Karata zake vizuri ana nafasi kubwa ya kuchukua Kiatu cha Ufungaji bora Afrika msimu huu kupitia Mashindani ya Klabu Bingwa Afrika.

Yanga mechi zake za awali itacheza ni Timu dhaifu sana ambayo ni Zalan FC hapo ndipo pa kujipigia Magoli zaidi ya 6.

Katika Mechi zote mbili dhidi ya Zalan FC Mayele ahakikishe anaondoka na Hatrick 2 jumla atakuwa na Magoli 6. Baada ya hapo katika Hatua itakayofuata kama wakikutana na Al Hilal ahakikishe mechi zote mbili anafunga goli 2 jumla atakuwa na Magoli 8.

Hata kama hatofunga katika hatua ya Makundi Magoli 8 yanaweza yakamtosha kubeba Kiatu. Mpaka mashindano yataisha sio rahisi mchezaji mmoja kufikisha Magoli 8 hivyo atajichukulia Kiatu kwa kucheza mechi za awali tu.

Kwa kuwa Yanga watakutana na Kibonde Zalan Mayele ana nafasi hiyo ya kufunga Magoli mengi. Mwaka 2014 Ngassa alikuwa miongoni mwa Vinara wa Magoli Afrika kwa kucheza mechi za awali tu akiwa na Magoli 7.

HAWA YANGA WAMEPANIA AISEE…WAAJIRI KOCHA ‘SHUSHU’ MAALUMU KWA MECHI YA CAF TU….KAZI YAKE ITAKUWA HII HAPA… WAKATI MADILI YAKIZIDI KUMMIMINIKIA ….MANDONGA AMTAKA TENA KAONEKA…ATAMBA SAFARI HII LAZIMA AUWEE MTU….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply