Home Azam FC ADEL ZRANE AIPA SIMBA BONGE LA KOCHA WA VIUNGO….AFUNGUKA DILI LILIVYOKUWA A-Z….

ADEL ZRANE AIPA SIMBA BONGE LA KOCHA WA VIUNGO….AFUNGUKA DILI LILIVYOKUWA A-Z….

Unamkumbuka yule kocha wa viungo Mtunisia ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa wa Simba katika ufanyaji wake wa kazi. Si mwingine bali ni Adel Zrane.


Zrane ni miongoni mwa makocha waliotumika kumshawishi kocha wa viungo wa Simba wakati huu, Karim Sbai kukubali kujiunga na klabu hiyo.

Sbai amesema kabla ya kukubali kuja kufanya kazi Simba alifanya mawasiliano na Zrane kumueleza anahitajika na klabu hii pamoja na mambo mengine ya msingi ambayo yote alimpatia majibu.

Amesema Zrane alinipatia majibu mazuri ndani ya Simba na kunieleza ni sehemu sahihi ya kufanya kazi na ni aina ya timu yenye malengo makubwa katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

“Wakati huo huo nimepata kazi hapa SImba kutokana na ukaribu wangu wa kufanya kazi kwa karibu katika nchi tofauti na kocha, Zoran Maki ambaye ndio amenileta hapa,” amesema Zoran Maki na kuongeza;

“Kikubwa nataka kuboresha na kuongeza utimamu wa miili ya wachezaji katika kikosi cha Simba ili muda wote kuwa tayari kwa ushindani katika kila mechi kwani hiyo ndio silaha ya kupata matokeo mazuri.

“Tangu nimefika hapa kuna kundi kubwa la wachezaji wamefanikiwa kupokea kile ambacho nimekuwa nikiwapatia katika kila zoezi.”
SOMA NA HII  KISA 'UMC WA MCHONGO JANA'...MKUU WA WILAYA AMTETEA MANARA...ADAI KAZI ALIYOFANYA HAIPO TFF...