Home Habari za michezo BAADA YA KUPIGIKA SANA ….MAN UTD WAFUFUKIA MBELE YA LIVERPOOL….’UZEE’ WAMPONZA RONALDO….

BAADA YA KUPIGIKA SANA ….MAN UTD WAFUFUKIA MBELE YA LIVERPOOL….’UZEE’ WAMPONZA RONALDO….

             


Hatimaye timu ya Manchester United wamefanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu wa 2022/23 baada ya kufanikiwa kuwabamiza mahasimu wao wa jadi, Liverpool kwa kipigo cha bao 2-1.

Mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake imepigwa katika Dimba la Old Trafford ikiwa mechi mbili zote za mwanzo za Ligi Manchester United alikuwa hajapata ushindi wala bao, kwani mechi zote alifungwa (mechi ya kwanza alifungwa na Brighton bao 2-1, mechi ya pili Man U akafungwa na Brtentford bao 4-0) hivyo mechi ya leo ndiyo imempa Man United pointi tatu za kwanza.

Mabao ya Manchester United yamefungwa na Jadon Samcho dakika ya 16 na Marcus Rushford dakika ya 53 huku bao la Liverpool likifungwa na Mohammed Salah dakika ya 82.

Ikumbukwe kuwa, Manchester United alikuwa hajamfunga Liverpool kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa kipindi cha miaka minne tangu mwaka 2018.

Vipigo vya hivi karibuni ni msimu uliopita ambapo Manchester alipigwa bao 4-2 katika mechi ya awali na mechi ya marudiano ya EPL, Man United alipigwa bao 4-0.

Mechi  ilikuwa ni ya kimbinu zaidi kwani Kocha Ten Hag alianza na vijana na kuamua kuwaacha nje Harry Maguire ambaye amekuwa akizungumzwa kutokuwa makini katika safu ya Ulinzi na Cristiano Ronaldo ambaye aliingia kipindi cha pili dakika ya 85.

Kwa matokeo hayo , Man United amekwea kutoka nafasi ya 18 mpaka nafasi ya 14 ya EPL huku Liverpool akishuka mpaka nafasi ya 16 baada ya kupata sare mbili na kupoteza mchezo mmoja huku akiwa hajashinda mchezo hata mmoja.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO SVEN ALIVYOIZIDI UJANJA SIMBA KWENYE DILI LA MIQUISSONE...LABDA WAJARIBU MSIMU UJAO...