Home Habari za michezo HIVI NDIVYO SIMBA WATAKAVYONUFAIKA NA MABILIONI YA M-BET…KILA MWAKA DAU LITAONGEZEKA MARA...

HIVI NDIVYO SIMBA WATAKAVYONUFAIKA NA MABILIONI YA M-BET…KILA MWAKA DAU LITAONGEZEKA MARA DUFU…


Club ya Simba SC leo imetangaza thamani ya Mkataba wao wa udhamini Mkuu na M Bet kuwa una thamani ya Tsh Bilioni 26, milioni 168 na elfu tano katika kipindi cha miaka 5.

Fedha hizo Simba itapokea kama ifuatavyo;

Katika mwaka wa kwanza Simba itapokea Bilioni 4 na milioni 670, mwaka wa pili Simba itapokea Bilioni 925, mwaka wa tatu Simba itapokea Bilioni 5 milioni 205 na laki Tano.

Mwaka wa nne Simba SC itapokea Bilioni 5 milioni 514 na elfu hamsini huku mwaka wa tano ambao ndio mwaka wa mwisho Simba itapokea kiasi cha Bilioni 5 milioni 853 laki nne na Elfu hamsini na tano.

Mbali na fedha hizo kuna stahiki mbali mbali ambazo Simba watakuwa wakizipata kulingana na matakwa ya Kimkataba baina yao na M-Bet.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA SKUDU KUSUGUA BENCHI ISHU KAMILI IKO HIVI