Home Habari za michezo RASMI….BOCCO NA SIMBA MAMBO YAMEFIKIA KIKOMO…ATETA NA MABOSI KUYAMALIZA…

RASMI….BOCCO NA SIMBA MAMBO YAMEFIKIA KIKOMO…ATETA NA MABOSI KUYAMALIZA…


Nahodha wa Simba, John Bocco ameiwahi Al Hilal baada ya kuwasili nchini Sudan ambapo wameenda kucheza mechi za kirafiki kujiandaa na michuano ya CAF na Ligi Kuu NBC.

Simba jana wamecheza mechi yao yua kwanza dhidi ya Asante Kotoko na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 huyku kocha msaidizi Seleman Matola akifunguka kuwa ni kipimo kizuri kwao huku akikiri kuwa yametoa nafasi ya kumsaidia kocha mkuu kupata picha harisi ya timu nzima.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kiliiambia kimedai kuwa Bocco ambaye amejiunga na kambi hiyo jana alishindwa kuongozana na wenzake kutokana na kuwa na kikao na viongozi.

“Bocco katua jana akiwa peke yake hakuweza kuambatana na wenzake kutokana na kuwa na kikao na viongozi natumai mambo yake yamekamilika ndio maana ameungana na timu” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  SABABU ZA SIMBA KUACHANA NA KIPA WAO MBRAZILI ZAWEKWA WAZI