Habari za michezo

SAKATA LA KUTOLEWA KWA MKOPO….AKPAN AJIFANYA HAJUI KINACHOENDELEA SIMBA….AJITETEA NA KAMBI YA MISRI…

admin August 22, 2022 1:37 pm


Kiungo mpya wa Simba, Victor Akpan anayetajwa kutakiwa kutolewa kwa mkopo Coastal Union, amesema hajui lolote juu ya dili hilo linaloelezwa kufanywa kwa sababu ya kocha Zoran Maki kutokubali kiwango chake tangu awe naye kambini Misri.

Akizungumza kiungo huyo mkabaji kutoka Nigeria alisema hajui lolote juu ya dili la mkopo kwa vile hajaelezwa na viongozi wala kocha. “Sijui kama nataka kutolewa kwa mkopo. Ujue nimesajiliwa hivi karibuni na nilikuwa kambini tangu timu ikiwa Misri.

“Kama jambo hilo lipo basi ni wewe (mwandishi) unayenieleza,” alisema Akpan aliyeisaidia na wenzake Coastal kufika fainali ya ASFC na kulala kwa Yanga.

Alipoulizwa kama yupo tayari kurudi Coastal, alisema ni mapema kwake kusema lolote.

PAMOJA NA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE NYINGI  YANGA….KIUNGO ALIYECHEZA EPL MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWAKE.. KISA KUFUNGA….’MZUNGU’ WA SIMBA AFUNGUKA JINSI ALIVYOPAMBANA NA MASHABIKI INSTGRAM…’WALIKUWA WANASUMBUA’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply