Home Azam FC STAA WA AZAM AULA UTEUZI TAIFA STRAS…NI BAADA YA KUFUNGA GOLI LA...

STAA WA AZAM AULA UTEUZI TAIFA STRAS…NI BAADA YA KUFUNGA GOLI LA KIDEONI…

 


Kocha Mdenmark, Kim Poulsen amemuongeza kiungo Tepsi Evans wa Azam FC kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Uganda Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary’s Kitende mjini Entebbe na mshindi atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.

Tepsie Evans ameinesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu mpya 2022/2023 akifunga mabao mawili katika meci mbili alizocheza mpaka sasa na kutoa pasi moja ya bao.

SOMA NA HII  MWENDA AKABIDHIWA MIKOBA YA AME