Home Habari za michezo WAKATI MAMBO YAKIZIDI KUWA MAMBO…BOCCO AVUNJA UKIMYA SIMBA…ADAI SIKU ZA MWANZO NI...

WAKATI MAMBO YAKIZIDI KUWA MAMBO…BOCCO AVUNJA UKIMYA SIMBA…ADAI SIKU ZA MWANZO NI TOFAUTI NA SASA…

[the_ad id="25893"]


Nahodha wa Simba, John Bocco amesema kulingana na maandalizi yao yalipotokea wiki mbili zilizopita hadi wakati huu mambo yote yanakwenda vizuri kama walivyokuwa wakihitaji.

Bocco alisema wapo kwenye eneo zuri kwa ajili ya kufanya mazoezi na maandalizi ya kutosha kwa ajili ya msimu ujao kutokana na utulivu mkubwa, vifaa vyote kupatikana kwa wakati pamoja na mambo ya msingi.

Alisema kila mchezaji aliyopo hapa kambini amefurahishwa na mazingira ya kambi na akili zao wote kubwa zimeelekea katika kupokea yale wanayopatiwa na benchi la ufundi.

“Mazoezi ya kila siku yamekuwa mazuri kwani wacgezaji tulivyokuwa siku za mwanzo ni tofauti kabisa na wakati huu tumeimarika mno kama ambavyo tulikuwa tunahitaji,” alisema Bocco na kuongeza;

“Hadi wiki moja iliyobaki kwa ajili ya mazoezi ikimalizika wachezaji watakuwa wameimarika zaidi na kila mmoja kutamani kwenda kuipigania Simba na kuhakikisha inapata mafanikio zaidi ya msimu uliyopita,” alisema Bocco na kuongeza;

“Wapenzi na mashabiki wa Simba wote wanatakiwa kuja Simba Day ili kuona hichi ninachoeleza hapa wachezaji wao tumeimarika kwenye maeneo mengi,”

“Tunaamini katika maandalizi haya tutakwenda kuwa na msimu mzuri huo ambao utaanza hivi karibuni,” alisema Bocco aliyeonekana kuwa na utimamuwa wa mwili wa kutosha na kufanya vizuri katika mazoezi ya jana ikiwemo kufunga mabao.

SOMA NA HII  NABI AFANYA UMAFIA DAR...MWENYEWE AFUNGUKA...MABOSI SIMBA WAAPA...SASA NI MWENDO KUGAWA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here